Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko TPF-NET Arusha yaonya jamii ya wafugaji zinazoendeleza ukatili wa watoto na wanawake
Habari Mchanganyiko

TPF-NET Arusha yaonya jamii ya wafugaji zinazoendeleza ukatili wa watoto na wanawake

Spread the love

 

MTANDAO wa Polisi wanawake wa Arusha kuelekea siku 12 za kupinga ukatili umeendelea na kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ambapo wametoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa jamii za kifugaji kata ya Lengijave wilaya ya Arumeru, mkoa wa Arusha na kuwaonya baadhi ya wananchi wa jamii ya kifugaji wanaofanya ukatili kwa wanawake na Watoto. Anaripoti Abel Paul, Jeshi la Polisi, Arusha … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP Zauda Mohamed ambapo amesema mtaandao huo umeendelea na kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia huku akibainisha kuwa wameona vyema kuangalia kundi hilo la jamii ya kifugaji.

Ameendelea kusema kuwa lengo ni kuendelea kutoa elimu na kutoa ujumbe huku akibainisha kuwa hapo awali kulikuwepo na changamoto za ukatili kwa jamii hiyo ambapo amesema wanaendelea kutoa elimu ilikuwajengea uwezo wa kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia kwa jamii hiyo ya kifugaji huku akitoa wito kwa jamii ya kifugaji kuchukia vitendo vya ukatili.

Kwa upande wake, Edina Rabiki mkazi wa kata ya Lengijave wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha licha ya kushukuru Jeshi hilo amesema kuwa jamii ya kifugaji ili kuwa na tabia ya kuoa Watoto wadogo ambapo ameushukuru mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha kwa namna ambavyo wameendelea kutoa elimu kwa makundi hayo ya kifugaji.

Naye Sajeti wa Polisi Upendo Molleli amewataka wananchi wa jamii hiyo ya kifugaji kuendelea kutoa taarifa ya watu wachache wanaofanya vitendo vya ukatili wa wanawake na mabinti wa kimasai kwa kufanyiwa vitendo vya ukatili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!