December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Bashiru ashutumiwa vikali

Spread the love

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimemtuhumu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ali kwamba anapotosha ukweli kuhusu kusinyaa kwa uchumi wa nchi.  Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Dorothy Semu, katibu mkuu wa chama hicho amesema, Dk. Bashiru anapaswa kuomba radhi Watanzania kwa kudai kuwa, uchumi wa Tanzania umekuwa kwa asilimia 7.8 kinyume na takwimu za Benki ya Tanzania (BoT) na Ofisi ya Taifa ta Takwimu (NBS), zinazoeleza kukua kwa asilimia 5.7.

Akizungumza na wanahabari leo Jumapili, tarehe 21 katika Makao Makuu ya chama hicho yaliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam, amedai kuwa kiongozi huyo amepotosha wananchi  kwa kuitetea takwimu zinazopikwa kwa maslahi ya kisiasa.

Amesema, wakati ACT-Wazalendo kinasimamia ukweli na kuweka wazi kuwa, hali ya uchumi kwa sasa hairidhishi. “Ukweli wetu unatufanya tusumbuliwe na dola.”

“Kufuatia uchambuzi wetu, kiongozi wa chama  chetu, Zitto Kabwe alikamatwa na Jeshi la Polisi akituhumiwa kukiuka sheria ya mtandao pamoja na sharia ya takwimu ya mwaka  2015, pia mimi na mwenyekiti wa chama Yeremiah Maganja, tulihojiwa  na kitengo cha makosa ya kifedha na takwimu,” amesema.

Semu ameeleza, licha kushikiliwa na kuhojiwa kwa viongozi wa chama hicho, Jeshi la Polisi limeendelea kushiklia komputa na simu ya Zitto.

Amesema, hali ya uchumi wa nchi kimekifanya chama hiko kipaze sauti iliyopelekea kushikiliwa na kuhojiwa kwa viongozi wao .

 

 

error: Content is protected !!