September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli amtimua uwaziri January Makamba

Spread the love

RAIS John Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa ya mabadiliko hayo imetolewa leo tarehe 21 Julai 2019 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa.

Taarifa ya Msigwa inaeleza kuwa, George Simbachawene ameteuliwa na Rais Magufuli kuirithi mikoba ya January kuanzia siku ya leo.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kwamba, Rais Magufuli amemteua Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo, akichukua nafasi ya Innocent Bashungwa, aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Magufuli amemteua Balozi, Dk. Martin Lumbanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).

https://twitter.com/jmakamba/status/1152798935355985922?s=21

Muda mchache baada ya kuvuliwa Uwaziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira na Rais John Magufuli, January Makamba atoa neno.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, leo tarehe 21 Julai 2019, January amesema ameyapokea mabadiliko hayo, kwa moyo mweupe.

Aidha, January amesema atazungumza zaidi siku zijazo, inagawa hakuweka bayana suala gani atakalolizungumzia.

“Kwa kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa 😊. Nitasema zaidi siku zijazo,” ameandika January katika ukurasa wake wa Twitter.

error: Content is protected !!