October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Bashiru apuliza kipyenga ubunge, udiwani kuanzia kesho 

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk. Bashiru Ally

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk. Bashiru Ally amewatangazia wanachama wa chama hicho wanaotaka kuwania ubunge, uwakilishi na udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 waanze kujipitisha pitusha kuanzia kesho Jumatano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Dk. Bashiru amesema hayo leo Jumanne tarehe 30 Juni 2020 wakati akipokea fomu za kuwania urais za Dk. John Magufuli Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.

“Kuanzia kesho nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani ziko wazi na wanaotaka kugombea wanaruhusiwa kuanza kujipitisha pitisha na kuulizia utaratibu siyo kufanya kampeni,” amesema Dk. Bashiru.

Amesema, wanaweza kujipitisha na kuulizia utaratibu wa jinsi ya kupata fomu ofisi husika za chama lakini si kufanya kampeni, kwani wakikiuka utaratibu Makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula atawashughulikia.

Dk. Bashiru amesema, shughuli ya uchukuaji na urejeshaji fomu za ubunge, uwakilishi na udiwani zitaanza kutolewa tarehe 14 hadi 17 Juni 2020.

Katika hilo, Rais Magufuli amesema, “kuanzia kesho ruksa wana CCM kupita pita,” huku wazingatie taratibu na maadili ya chama na watakaoshindwa wawaunge mkono watakaopewa ridhaa.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI ONLINE & MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

error: Content is protected !!