Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari Dk. Amani Karume: Maendeleo ya wananchi si majengo tu!
Habari

Dk. Amani Karume: Maendeleo ya wananchi si majengo tu!

Spread the love

 

RAIS mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume ameeleza kufarijika kuona namna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi namna wanavyoshirikiana kuwaleta kuhamasisha uwekezaji nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Amesema viongozi hao wameshika pahala ambapo waliotangulia wamewaachia na wanafanya juhudi kuendeleza maendeleo ya nchi.

Aidha, amesema maendeleo ya nchi sio majengo tu bali maendeleo ya nchi ni maendeleo ya wananchi wenyewe.

Dk. Karume ametoa kauli hiyo leo tarehe 7 Disemba 2021, Visiwani Zanzibar katika ufunguzi wa kongamano la maonesho ya bidhaa za viwanda.

Kongamano hilo ni maalumu katika kujadili changamoto na mafanikio ya maendeleo ya uwekezaji kwa kipindi cha miaka 60 tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961.

Dk. Karume amesema katika mkutano huo ambao wajumbe wametoka sehemu mbalimbali, amefarijika kuona wenyeji wengi wapo.

Amesema ujio wa wenyeji utapata nafasi kujifunza kutoka kwa wageni ambao tayari wana utaalam wa ziada.

“Viongozi hao wameshika pahala ambapo waliotangulia wamewaachia na wanafanya juhudi kuendeleza maendeleo ya nchi. Maendeleo ya nchi sio majengo tu, maendeleo ya nchi ni maendeleo ya wananchi wenyewe.

“Juhudi wanazochukua sasa ni kukaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje waje wawekeze ili kukuza uchumi ambao ukikua ndipo maendeleo ya nchi huonekana. Ajira zitapatikana na wananchi wataishi vizuri zaidi.

“Ninafarijika kuona kwamba hatua hizi zinazochukuliwa wakati huu na wananchi wenyewe wanapata nafasi ya kushiriki,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!