Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CUF yazindua sera mpya kuondoa umasikini
Habari za Siasa

CUF yazindua sera mpya kuondoa umasikini

Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba
Spread the love

 

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimezindua sera mpya ya kipato cha msingi kwa wananchi wote (Universal Basic Income), inayolenga kupunguza makali ya ugumu wa maisha kwa wananchi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Sera hiyo imezinduliwa jana tarehe 20 Agosti 2023 na Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba, katika mkutano wa hadhara wa chama hicho, uliofanyika Mbagala, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu, leo tarehe 21 Agosti 2023, Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma CUF, Mhandisi Mohammed Ngulangwa, amesema sera hiyo itatekelezwa wakati chama chake kitakapoingia madarakani.

Mhandisi Ngulangwa ameeleza kuwa, CUF ikifanikiwa kuingia madarakani, itatumia rasilimali za nchi kupata fedha za kufanikisha utekelezaji wa sera hiyo, ambapo Serikali yake itatoa fedha za ruzuku kwa awamu kwa wananchi wenye uhitaji.

“Jambo hili ni jepesi, kama tungetumia vyema rasilimali zetu, mfano misitu, madini, gesi, maziwa, mito, bahari, ingepelekea kukuza uchumi na kuona namna gani tungetumia rasilimali tulizonazo ili kila mtanzania apate kipato cha msingi,” amesema Mhandisi Ngulangwa.

Mhandisi Ngulangwa amesema, kinachopelekea Serikali zilizopita kushindwa kupunguza idadi ya wananchi wanaoishi katika wimbi la umasikini, ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma, ufisadi na matumizi yasiyo na tija.

“Kilichopo hatutumii vizuri rasilimali tulizonazo kama nchi na zinapotumika wachache wananufaika, CUF tutakapoingia madarakani tutazitumia vizuri kuhakikisha kila mtu anakuwa na kipato kisha kukikuza kiwe kikubwa,” amesema Ngulangwa na kuongeza:

“Mfano marehemu Muamar Ghadafi wa Libya, alitumia mafuta kutoa ruzuku kwa wananchi wake, lakini sisi tuna rasilimali nyingi tunashindwa kufanya hivyo kwa sababu hakuna matumizi mazuri.”

Jana wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara, Prof. Lipumba alisema CUF ikiingia madarakani itajenga mazingira yatakayokuza uchumi wa nchi na pato la taifa kwa wastani wa asilimia 10 kila mwaka.

Prof. Lipumba alisema kwa sasa wananchi wengi wana hali ngumu ya maisha kutokana na sera zilizopo kutokuwa rafiki kwenye ukuaji uchumi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!