April 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Corona: Mbowe siku 14 karantini

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), sasa yupo karantini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amechukua hatua hiyo yeye mwenyewe na familia yake. Ni baada ya mtoto wake Dudley kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19). Kwa sasa Dudley anaendelea vizuri katika Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Clouds FM katika kipindi cha Jahazi tarehe 25 Machi 2020, Mbowe amesema, amejiweka karantini jijini Dodoma huku akiendelea na shughuli pia kuwasiliana na watu wake kupitia mtandao.

Amesema, amechukua hatua hiyo ikiwa hatua madhibiti kusambaa na kusubiri majibu, kwamba kama naye ana maambukizi hayo ama la “nasubiri majibu kujua kama nina maambukizi ama la.”

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Kilimanjaro, amesema “unapokuwa na mgonja wa corona, jamii inakutazama kwa hofu na kwamba, kutokana na hivyo ni vema kujitenga kwa siku 14 huku nikisubiri majibu.”

Amesema, amekutana na watu wengi kabla ya kujiweka karantini, na kwamba ni jambo la kumuomba Mungu asiwe ameambukizwa.

error: Content is protected !!