Tuesday , 5 December 2023
Home Kitengo Maisha Afya Mgonjwa wa kwanza wa corona Tanzania apona
Afya

Mgonjwa wa kwanza wa corona Tanzania apona

Isabela Mwampamba
Spread the love

ISABELA Mwampamba (46), mgonjwa wa kwanza kupatikana na virusi vya corona (COVID-19) nchini Tanzania, amepona na yupo huru kuungana na familia yake. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya amesema, muda wowote kuanzia sasa Isabela ataruhusiwa kuendelea na shughuli zake huku akitoa angalizo la kutonyanyapaliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo tarehe 26 Machi 2020, Ummy amesema Isabela baada ya kupata vipimo vyote, vipimo vimeonesha kwamba yupo salama.

Tarehe 16 Machi 2020, Isabela alitangazwa kuwa mgonjwa wa kwanza kupatikana na virusi vya corona nchini, pia serikali ilianza ‘msako’ kwa wote  waliokuwa karibu na Isabela ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.

Pia Ummy ameseama mpaka sasa, Tanzania ina jumla ya wagonjwa 13 ambapo kati yao wanane ni Watanzania na watano ni wageni na kwamba Arusha (2), Dar es Salaam (8),  Zanzibar (2) na  Kagera (1).

Amesema, wagonjwa 12 wote waliambukizwa nje ya nchi na mmoja aliambukizwa na mmojawao kati ya hao 12.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Majaliwa aipongeza GGML mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveWaziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Kampuni ya Geita Gold Mining...

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaMichezo

GGML yatoa milioni 17 kung’arisha ATF Marathon

Spread the loveKATIKA kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kukabiliana na maambukizi...

Afya

‘Ambulance’ yawarejeshea tabasamu wananchi Mkuyuni

Spread the loveWananachi wa  Tarafa ya Mkuyuni, Halmashauri ya Morogoro mkoani Morogoro,...

error: Content is protected !!