Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mkutano ‘kumng’oa’ Meya Iringa waitishwa
Habari za Siasa

Mkutano ‘kumng’oa’ Meya Iringa waitishwa

Alex Kimbe, Meya wa Manispaa ya Iringa
Spread the love

MKAKATI wa muda mrefu unaoondeshwa na wabunge pia madiwani kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumng’oa Meya wa Manispaa ya Iringa, sasa umeshika kasi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa…(endelea).

Tayari madiwani hao wamepokea wito wa kuhudhuria kikao kilichoitishwa kwa haraka na Hamidu Njovu, Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa. Kikao hicho kimechopangwa kufanyika kesho tarehe 26 Machi 2020 katika ukumbi wa mikutano wa manispaa hiyo.

“Napenda kuwaarifu kuwa mkutano wa baraza maalum la madiwani litafanyika tarehe 26 .03.2020 siku ya Alhamis kuanzia saa 02:00 asubuhi…,” umeeleza wito huo na kuongeza:

“Kwa barua hii mnaalikwa rasmi kuhudhuria mkutano huo bila kukosa…”

Mkakati wa wabunge wa CCM Iringa kupanga njama za kumng’oa Alex Kimbe, Meya wa Manispaa ya Iringa ulishika kasi baada ya Isaya Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam kumkaba koo wakitaka kumtimua. Isaya aligoma baada ya taatibu kushindwa kukamilika

Meya Kimbe (Chadema), alianza kusakamwa na baadaye kupewa barua ya kujieleza kutokana na kuvishwa tuhuma nne.

Tuhuma hizo ni ukosefu wa adabu, matumizi mabaya ya madaraka, matumizi mabaya ya rasilimali za halmashauri na vitendo vya rushwa.

Tarehe 2 Machi 2020, Meya Kimbe alisema amepokea barua iliyobeba tuhuma hizo za kupikwa kwa sababu maalum za kisiasa.

“Nitapeleka barua kwa mkurugenzi wa manispaa ili nimweleze na kumkumbusha vyombo vya usalama na watendaji wake taratibu na kanuni za kumtoa Meya madarakani wamezikosea,” alisema.

Meya Kimbe alisema, CCM, kimekosa fursa kwa wananchi na sasa kinatumia hila kukabili maeneo yanayoongozwa na wapinzani ikiwemo Manispaa ya Iringa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

error: Content is protected !!