Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chongolo awachongea wakuu wa mikoa, wilaya kwa Rais Samia
Habari za SiasaTangulizi

Chongolo awachongea wakuu wa mikoa, wilaya kwa Rais Samia

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo
Spread the love

KATIBU Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kutoa kauli kuhusu wakuu wa wilaya na mikoa ambao wameshindwa kuthibiti kikundi kidogo cha wafugaji ambao wanaendesha shughuli za ufugaji katika maeneo ambayo yamezuiliwa kisheria. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema jambo hilo haliashirii mazuri huko mbele hasa ikizingatiwa CCM imepewa dhamana ya kuisimamia Serikali.

Chongolo ametoa kauli hiyo leo tarehe 8 Agosti 2023 wakati akihutubia katika kilele cha sherehe za wakulima nanenane zinazofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Amesema kumeanza kutokea dalili ya baadhi ya wafugaji wasio waaminifu kuanza kuendesha ufugaji wenye madhara kwa wengine ikiwemo kupeleka mifugo kwa wakulima, mashamba na maeneo mengine

Amesema mifugo inayolalamikiwa kukiuka taratibu inatokana na kuna kikundi kidogo cha watu wanaokiuka taratibu, sheria wanapeleka mifugo kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi kutumika kwa ufugaji, matokeo yake imeanza kuwa na malalamiko kwenye maeneo mengi nchini.

“Kote kwenye malalamiko hayo kuna viongozi wanaokuwakilisha huko wanaosimamia sheria kwa niaba yako. Ni vema hili jambo likatolewa kauli dhabiti kwamba mikoa na wilaya ambayo kuna changamoto ambazo zinaanza kuleta viashiria vya migogoro kwa makundi haya.

“Huyo mtu ni dhahiri hajaamua kufanya kazi yake na kutimiza wajibu wake.  Na jambo hili si jambo la kuliendeleza na kulilea kwa sababu lina madhara mbele yake,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!