May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chelsea wamweka kikaangoni Arteta

Spread the love

 

KIPIGO cha bao 2-0 kutoka kwa mabingwa wa Ulaya, Chelsea, kimemuweka kikaangoni Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta baada ya mashabiki kuutaka uongozi wa klabu hiyo kumtimua. Anaripoti Mintanga Hunda, TUDARCo … (endelea).

Arsenal ikiwa Uwanja wa Emirates jana tarehe 22 Agosti, 2021 ilikubali kunyooshwa kwa mabao 2-0 na kupoteza kwa mara ya pili mfululizo kwani katika mechi ya ufunguzi wa Ligi kuu England Arsenal ilikubali kichapo cha bao 2-0 mbele ya Brentford.

Kufuatia matokeo hayo baadhi ya mashabiki wameanzisha vuguvugu la kumtaka kocha huyo atimuliwe kwa kuwa ameshindwa kurejesha makali ya timu hiyo.

Mikel Arteta

Wakati hayo yakijiri Chelsea wameeleza kuchekelea kumtungua mtani yaani Arsenal ikiwa ni ushindi wa pili mfululizo tangu ligi hiyo ianze.

Katika mchezo huo wa jana Chelsea walipata mabao yake kupitia mshambuliaji wao mpya kutoka klabu ya Inter Milan ya Italia, Romelu Lukaku na mchezaji wao chipukizi Rice James na kufanikiwa kuondoka na alama tatu mkononi wakiwa ugenini

Kupitia ushindi huo kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel amesema huo ni mwanzo mzuri kwenye ligi kwani inawajengea hali kubwa ya kujiamini.

error: Content is protected !!