Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Washtakiwa wenzake Mbowe wadai walazimishwa kutoa maelezo
Habari za Siasa

Washtakiwa wenzake Mbowe wadai walazimishwa kutoa maelezo

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu
Spread the love

 

WASHITAKIWA watatu wenzake na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, kwamba maelezo yaliyosomwa na upande wa mashtaka mahakamani hapo, yakidaiwa kuwa yao, waliyatoa bila hiyari yao. Anaripoti Victoria Mwakisimba, TUDARCo na Regina Mkonde…(endelea).

Wamesema hayo leo Jumatatu, tarehe 23 Agosti 2021, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi, ilipoitwa kwa ajili ya upande wa mashtaka kuwasomea watuhumiwa hao maelezo ya awali.

Washitakuwa hao Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Abdallah Ling’wenya wamedai waliyatoa maelezo hayo kwa kulazimishwa kwa kipigo.

Washtakiwa hao walitoa madai hayo, baada ya Hakimu Simba kuwahoji kama wana neno lolote juu ya maelezo yanayaodaiwa kuwa ya kwao, ambayo yaliyosomwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Penetreza Kitale.

Hakimu Simba alipomuuliza mshtakiwa wa kwanza, Bwire alijibu akidai kwamba alichukuliwa maelezo hayo bila ya uwepo wa wakili wake, baada ya kupigwa na kupatiwa mateso makali.

“Malelezo yaliyosomwa nilichukuliwa bila wakili wangu. Maelezo yalichukuliwa baada ya kupatiwa mateso Tazara, mateso makubwa na ya kufedheheshwa. Hivyo hayakuwa maelezo ya hiari,” amedai Bwire.

Baada ya mshtakiwa huyo wa kwanza kujibu hivyo, Hakimu Simba alimuuliza mshtakiwa wa pili, Lingw’enye, ambaye naye pia alidai “maelezo niliyochukuliwa Polisi yalichukuliwa baada ya kunyanyaswa, maelezo niliyoyatoa hayakuwa ya hiari yangu mheshimiwa.”

Hakimu Simba aliendelea kumuuliza mshtakiwa wa tatu, Kasweka, ambaye alidai hayakuwa maelezo yake kwa madai alilazimishwa kuyasaini bila kuyasoma.”

“Yalikuwa siyo maelezo yangu, nilisurubiwa na kupigwa wala sikuyasoma, nimeyasikia hapa (mahakamani). Nilichoambiwa ni kusaini tu. Nilipigwa, kuteswa na pia maelezo haya nimesikia hapa, Polisi sikupewa kuyasoma nilipewa nisaini tu.”

Ilipofika zamu ya mshtakiwa wa nne ambaye ni Mbowe, Hakimu Simba alimuuliza kama ana neno, ambapo Wakili upande wa utetezi, Peter Kibatala alijibu kwa niaba yake akisema mteja wake hana la kusema.

Awali, Wakili Kitale akisoma maelezo ya washtakiwa hao, alidai Mbowe alikataa kutoa maelezo wakati anahojiwa akisema atatoa maelezo yake mahakamani.

Wakili Kitale alisema kuwa, Mbowe aligoma kutoa maelezo hayo tarehe 22 Julai 2021, alipokuwa anahojiwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, mkoani Dar es Salaam.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Simba aliihamisha kesi hiyo katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, yenye mamlaka ya kuisikiliza.

Hakimu Simba aliihamisha kesi hiyo baada ya mahakama hiyo kukamilisha taratibu za usikilizwa wa awali.

Wakili Kibatala amesema kesi hiyo itaanza kusikilizwa katika Mahakama Kuu, baada ya mahakama hizo mbili kuwasiliana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!