May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wanne wajeruhiwa ajali ya basi Kibaha

Spread the love

 

WATU wanne wamejeruhiwa na wengine 40 kunusurika kifo baada ya kutokea ajali ya basi la kampuni ya Sauli eneo la Picha ya Ndege Kibaha mkoani Pwani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema ajali hiyo imetokea leo Jumatatu tarehe 23 Agosti, 2021 saa 6:45 asubuhi.

Amesema dereva wa basi hilo ambaye jina lake halikupatikana mara moja alilielekeza pembezoni mwa barabara ili kukwepa kugongana uso kwa uso na lori lillokuwa likitokea mbele yake.

Kamaanda Nyigesa amesema kuwa dereva wa basi hilo alikuwa akilipita gari lililokuwa mbele yake na baada ya kufanikiwa, aliona lori la mchanga ndipo aliamua kulikwepa.

Alisema kuwa majeruhi hao wamewahishwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi ambapo walipatiwa matibabu kisha kuruhusiwa.

error: Content is protected !!