June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ukinunua chapati zaidi ya nne, unakamatwa

Chapati

Spread the love

 

JESHI la Polisi nchini Uganda limesema mtu yeyote atayenunua chapati tano au zaidi Kaskazini mwa nchi hiyo huenda akakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya usalama. Anaripoti mwandishi Wetu … (endelea)

Kamishna wa Polisi mkoa wa Karamoja nchini humo, Michael Longole alifichua kuwa ripoti ya ujasusi ilionesha baadhi ya watu wanaonunua chapati kwa wauzaji wa barabarani walikuwa wanazitumia kwenda kuwashibisha majambazi waliojificha vichakani.

Akizungumza na Kituo cha utangazaji cha serikali cha Uganda, Radio Network, Longole alidai baadhi ya watu walikuwa wakinunua chapati ili kuwalisha wezi wa ng’ombe waliojificha kwenye vichaka vya wilaya ya Mororo.

“Sasa tunamkamata mtu yeyote anayenunua chapati zaidi ya tano na tunamhoji kwa nini ananunua chapati hizo zote na anazipeleka wapi kwa sababu tumepata habari kwamba wanaonunua chapati nyingi huwapelekea majangili waliojificha vichani,” alisema.

Longole alisema ikiwa usambazaji wa chakula kwa wahalifu utakomeshwa, watalazimika kurejea nyumbani na kusalimisha silaha zao haramu kwa serikali.

Hata hivyo, wakazi walikuwa na maoni tofauti na agizo huku wengi wao wakisema hiyo sio dawa ya maofisa hao kupambana na wahalifu hao.

error: Content is protected !!