Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yatoa msimamo sakata la bandari, yataka walioshiriki wajiuzulu
Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatoa msimamo sakata la bandari, yataka walioshiriki wajiuzulu

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewataka watu waliohusika katika uandaaji mkataba wa ushirikiano wa kiserikali kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai, kuhusu uendeshaji bandari, wajiuzulu kwa madai kuwa wameingia makubaliano yasiyokuwa na maslahi kwa taifa. Anariupoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 14 Julai 2023, jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, akitangaza maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho, kuhusu mkataba huo.

Mbali na wito wa kutaka waliohusika na mkataba huo kujiuzulu, Mbowe amesema Chadema kinaunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na wananchi kupinga mkataba huo ambao utatekelezwa na Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kwa kushirikiana na Kampuni ya DP World kutoka Dubai.

Mbowe amedai, mkataba huo una dosari kwa kuwa haurekebishiki, huku akitoa wito kwa Bunge kufuta azimio lake lililopitisha hivi karibuni, kuuridhia.

Hata hivyo, mapema leo timu iliyoshiriki majadiliano kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uandaaji mkataba huo, imetoa ufafanuzi ikisema mkataba huo hauna dosari na maslahi ya taifa yamezingatiwa.

Imesema asilimia 80 ya mapendekezo yanayotolewa sasa kuhusu marekebisho yake, yatafanyiwa kazi kwenye mikataba ya utekelezaji itakayoingiwa hapo baadae.

1 Comment

  • Nina mashaka mkataba huu hautofautiani na richmond . Ni mipango ya kifisadi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

error: Content is protected !!