February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Chadema wateua wa kupambana na Waitara, Kalanga

Kamati Kuu ya Chadema

Spread the love

CHAMA cha Chadema kimeteua wagombea ubunge katika majimbo matatu yaliyoachwa wazi baada ya wabunge wawili kujiuzulu na mmoja kufariki. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Uteuzi huo umefanywa leo tarehe 17 Agosti, 2018 na Kamati Kuu ya Chadema na kutangazwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Chadema, Tumaini Makene.

Kamati hiyo iliyoketi kwa muda wa siku mbili, imemteua Asia Msangi kuwa mgombea kwenye Jimbo la Ukonga, Yonas Laiser amechaguliwa kukiwakilisha chama hicho katika jimbo la Monduli na Amina Saguti ameteuliwa kugombea Korogwe Vijijini.

Katika majimbo hayo, mawili yalikuwa yanashikiliwa na makada wa Chadema akiwemo Mwita Waitara (Ukonga) na Julius Kalanga (Monduli) ambao hivi karibuni walijivua uanachama wa chama hicho na kujiuzulu ubunge.

error: Content is protected !!