December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli aula SADC

Rais John Magufuli

Spread the love

DK. John Magufuli, Rais wa Tanzania ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo tarehe 18 Agosti, 2018 na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Rais Magufuli ameteuliwa na Wajumbe walioshiriki katika mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliofanyika Windhoek nchini Namibia kuanzia tarehe 17 hadi 18 Agosti mwaka huu.

Rais Magufuli atashikilia wadhifa huo kuanzia mwezi Agosti 2018 mpaka Agosti 2019.

Kufuatia uteuzi huo, Dk. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atapewa rasmi jukumu la Uenyekiti wa SADC katika Mkutano mkuu ujao wa 39 utakaofanyika Tanzania mwezi Agosti 2019.

error: Content is protected !!