Thursday , 18 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Taasisi za mbegu zatakiwa kuweka mikakati ya kuinua kilimo
Habari Mchanganyiko

Taasisi za mbegu zatakiwa kuweka mikakati ya kuinua kilimo

Baadhi ya mifuko ya mbegu bora za kisasa
Spread the love

NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba amezitaka Taasisi zinazojihusisha na masuala ya mbegu nchini kuweka mipango mikakati wa miaka minne itakayoendana na mpango wa kufanya mapinduzi makubwa ya kilimo (ASDP II) ili kuinua kilimo nchini. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Mgumba alisema hayo jana wakati akiongea na wafanyakazi wa Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) ambapo alizitaja Taasisi hizo kuwa ni pamoja na TOSCI alisema, Wakala wa usambazaji mbegu nchini (ASA) na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nchini (TARI).

Alisema ikiwa Taasisi hizo zitaweka mikakati thabiti ya upatikanaji wa mbegu bora kwa wingi na kwa wakati kwa mkulima, utoaji wa elimu ya kilimo bora katika mazao mbalimbali yanayolimwa nchini, matumizi ya udongo na mbolea, na kuonyesha namna mkulima anavyoweza kupata faida baada ya kuboresha kilimo chake na kuenda sambamba na wakati uliopo sasa.

Hivyo alisema, elimu na mpango mkakati huo utamsaidia mkulima kuona namna ya kuongeza uzalishaji kufuatia kuwa na uhakika kupata kufanya kilimo chenye uzalishaji mzuri huku akiziagiza taasisi hizo kuona haja ya kufuatilia masoko katika nchi mbalimbali duniani kwa manufaa ya wakulima lengo likiwa ni kumfanya mkulima kuwa na uhakika wa masoko.

Mgumba alisema, Rais John Magufuli alizindua mpango wa ASDP II kufuatia mpango wa ASDP I kuonekana haukufanya vizuri kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa mbegu za uhakika na kwamba ASDP II imewekewa mikakati hiyo ili isije kushindwa kufanya vizuri lengo likiwa ni kuinua uchumi katika sekta ya kilimo nchini.

Alisema, mpango huo wa ASDP II umepangwa kutekelezwa katika awamu mbili za miaka mitano mitano kuanzia 2017/18 hadi 2021/22 ambapo alizitaka Taasisi hizo kuweka mikakati yake sawa itakayoweza kutekelezeka na kuinua asilimia 65 ya watanzania ambo wanategeme kilimo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya TOSCI, Patrick Ngwediagi alisema wamefanikiwa kuongeza utambuzi wa mbegu zenye ubora kutoka mbegu Tani 10,000 mwaka 2014 hadi kufikia mbegu bora Tani 32,000 mwaka 2017 zinazoweza kutumiwa na wakulima kwa mazao mbalimbali hapa nchini.

Ngwediagi alisema, wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya uelewa mdogo wa mkulima kuhusu matumizi ya mbegu bora licha ya kuendelea kutoa elimu, muonekano wa mbegu bandia (Feki), upungufu na ukosefu wa vitendea kazi ikiwemo magari, majengo na wafanyakazi hasa mikoani.

Hivyo Ngwediagi TOSCI inampango wa kuingiza mfumo wa lebo za kudhibiti ubora za mtindo wa kukwangua kama vocha ili kumrahisishia mkulima kujua kama mbegu aliyonunua imekaguliwa lini na ina ubora kiasi gani kupitia simu yake tofauti na ilivyo kwa sasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

Habari Mchanganyiko

Serikali yatoa ajira watumishi 46,000, yatangaza utaratibu mpya kuajiri

Spread the loveSERIKALI imetangaza nafasi za ajira za watumishi wa umma 46,000...

error: Content is protected !!