Friday , 2 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema watetea wabunge wasiwe ombaomba
Habari za SiasaTangulizi

Chadema watetea wabunge wasiwe ombaomba

Spread the love

VICENT Mashinji, Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amelituhumu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuvunja Katiba ya nchi na kuomba fedha kwa Serikali bila kufuata utaratibu, anaandika Irene Emmanuel.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mashinji amesema, Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila ameandika barua kwenda kwa Waziri Mkuu na nyingine kwa Katibu Mkuu Hazina akiomba fedha ajili ya amatumizi mbalimbali.

Serikali imeshatoa Shilingi bilioni saba kwa ajili ya Bunge, lakini huko nyuma tumeshuhudia ukiukwaji wa Katiba baada ya serikali kununua ndege, kujenzi wa kiwanda cha ndege Chato bila kufuata utaratibu.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara yetu ya 73 inasema kuwa wabunge wote wa aina zote watashika madaraka yao kwa mujibu wa katiba hii na watalipwa mshahara, posho, na malipo mengine kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

“Tatizo hapa siyo kupeleka pesa bungeni, tatizo ni kufuata utaratibu, Bunge ndilo linalopitisha bajeti iweje leo linaomba omba? Bunge limevunja ibara ya 137/3A na B kwa kuomba fedha za ziada nje ya bajeti yake iliyoidhinishwa na Bunge bila kufuata utaratibu wa kuipitisha bungeni,” ameongeza Mashinji.

Mwaka wa Fedha 2016/17 wabunge wamekuwa wakiondoka bungeni bila kulipwa stahiki zao moja ya sababu iliyosababisha Dk Kashilila kuandika barua ya kuomba pesa kwa Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

error: Content is protected !!