Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema wataka wachunguzi wa kimataifa sakata la MO
Habari za Siasa

Chadema wataka wachunguzi wa kimataifa sakata la MO

Spread the love

CHAMA cha Chadema kimeitaka serikali kuruhusu wachunguzi wa kimataifa kuchunguza tukio la kutekwa kwa Mfanyabiashara, Mohammed Dewji ‘MO’ lililofanywa  na watu wasiojulikana tarehe 11 Oktoba 2018 katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Wito huo wa Chadema umetolewa leo tarehe 16 Oktoba 2018 jijini Dar es Salaam na Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Godbless Lema ambaye pia alimtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kuacha mara moja kuzuia watu kujadili tukio hilo.

Lema amedai kuwa, kitendo cha familia ya Dewji kutangaza dau nono la Sh. 1 bilioni kwa mtu atakayetoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa MO, kinaashiria kuwa mfanyabisahara huyo hajatekwa na watu wa kawaida wenye shida ya fedha, kwani ingekuwa hivyo waliomteka wangewasiliana na familia yake kwa ajili ya kudai malipo ili wamuachie huru.

Amedai kuwa, ili serikali kujivua lawama ya kuhusika na matukio ya watu kupotea hususan la Mo, iruhusu wachunguzi wa kimataifa kwa kuwa familia yake ina uwezo wa kulipia wachunguzi kutoka taifa lolote duniani.

“Sisi kama chama tunasema kwamba ili serikali ijivue kwenye mashaka ya muda mrefu ambao tunayo dhidi yake, namna peke yake ya kushughulikia suala hili ni kuruhusu wapelelezi wa kimataifa waingie waje wafanye uchunguzi, wasipofanya hivyo hatuwezi kukosa kutilia mashaka mifumo kwa sababu ya hali ilivyo.

Lakini juzi mmesikia Kangi amesema kwamba Tanzania ina uwezo wa kuyakabili mambo haya bila msaada wa nje, kuhitaji msaada wa kiupelelezi si weakness ‘udhaifu’, ni busara kwa ajli ya kutoa confidence ‘ujasiri’ na kuonyesha credibility  ‘uwajibikaji’ ya taifa na utawala dhidi ya tuhuma zake kwamba  pengine unaweza unafanywa na ajent wa serikali,” amesema.

Lema ameitaka serikali kutoona aibu kushirikiana na wapelelezi wa kimataifa katika kufanya uchunguzi wa kutekwa kwa Mo Dewji ili kuondoa athari zitakazoweza kusababishwa na tukio hilo ikiwemo kushuka kwa uchumi wa nchi.

“Huyu aliyetekwa anakontribute ‘anachangia’ 3.5% ya pato la nchi kwa mwaka, anaajiri watu 23,000 anaweza akapotea hivi, ni nani katika nchi hii yuko salama isipokuwa viongozi wakuu wa serikali, leo Mo ameondoka na mtu maarufu anayemiliki  timu ya mpira yenye fans ‘mashabiki’ wengi, jana rais alikuwa anapokea wakimbiza  mwenge nilitarajia kungekuwa na taarifa ya serikali,

magazeti makubwa duniani yameandika, matokeo yake kwenye uchumi ni makubwa mno, kama nchi hii biashara zetu zingekua zimeorodheshwa  kwenye soko la hisa mngeona kiasi gani shilingi  ingekuwa inaporomoka na uchumi kwa ajili ya jambo hili, leo hizi habari zinaenda kwenye bilionea klabu hawa ndio wanashawishi wawekezaji,  wanaona Mo ametekwa,” amesema.

Katika hatua nyingine, Lema aliitaka jamii, taasisi za biashara, kidini,  na viwanda kutoka hadharani kupaza sauti zao kuhusu tukio hilo.

“Wito kwa jamii viongozi wa dini, taasisi ya biashara na zinazoshughulika na viwanda watoke hadharani, Mo ni moja ya memba wa taasisi zinazoshughulika na taasisi za biashara na viwanda watoke waseme kwa sauti wasipofanya hivi mwengine atachukuliwa, rai yetu wakina Reginald Mengi watoke,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!