Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yakomaa Umeya wa Jiji Dar, serikali yasalimu amri
Habari za SiasaTangulizi

Chadema yakomaa Umeya wa Jiji Dar, serikali yasalimu amri

Spread the love

VUTA nikuvute kwenye Uchaguzi wa Naibu Meya wa jiji la Dar es salaam jana imesababisha serikali kuahirisha uchaguzi huo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Tarehe ya uchaguzi huo itatangazwa baadaye baada ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na yule wa Ubungo, Saed Kubenea kuapa kutodhuliwa.

Kilichosababisha vuta nikivute kwenye uchaguzi huo kwa baadhi ya vipengele vilivuoonekana kuwa n maslahi kwa upande mmoja.

Moja ya vipengele hivyo ni kutokukubaliwa kwa hati ya mgombea wa nafasi hiyo aliyetokea (UKAWA) kupitia Chama Cha Wananchi (CUF).

Katika mkutano huo baadhi ya wajumbe akiwemo Mdee na Kubenea wakiingia kwenye malumbano ya maneno na Mkurugenzi wa Jiji, Sipora Riama kuhusu hati ya mgombea huyo.

“Tunaomba hoja iliyotolewa na mjumbe Ndugulile aipokee Mkurugenzi na aseme ameikubali ili twende mbele, mheshimiwa ndugulile tumuulize Mkurugenzi amekubali kuja na utaratibu mpya kwenye kikao kijacho”, alisema Kubenea.

“Kwanini unaingilia majukumu yangu, huyu naye ni (Meya wa jiji) ana maslahi hawezi kutoa miongozo, mimi nina wanasheria hapa, maafisa utumishi ili kusimamia uchaguzi na miongozo mimi ndo natoa”, alisema Sipora wakati akizungumza kwa sauti kwenye kikao hicho.

“Nimshukuru Mheshimiwa Ndugulile, kwa kuwa tumekubaliana kuhairisha kikao, naomba UKAWA kupitia chama cha wananchi CUF kipate haki yake ya kupata mgombea wake, tunaomba kikao kinachokuja ajenda moja wapo iwe ni uchaguzi”, alisema Mdee kwa kumalizia.

Awali Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile alitoa ushauri wa kuhairishwa kwa ajenda ya uchaguzi kwenye kikao hicho, hoja ambayo ilikuja kukubaliwa mwishoni mwa kikao.

“Kikao chetu kimedumu kwa zaidi ya saa 4 kitu ambacho nakiona hapa, mjadala huu hautafika mwisho, naomba tuhairishe ajenda ya uchaguzi mpaka siku nyingine”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!