December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Manara achomoka sakata la MO

Haji Manara

Spread the love

MKUU wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara pamoja na watu 19 waliokuwa wanashikiliwa kutokana na sakata la kutekwa kwa Mfanyabishara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’,  wamechwa huru kwa dhamana. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa inaeleza kuwa Manara na wenzake wameachwa kwa dhamana usiku wa jana tarehe 15 Oktoba 2018.

Manara aliyesota rumande tangu Oktoba 12 mwaka huu hadi usiku wa jana, alikamatwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kusambaza taarifa za tukio la kutekwa kwa Mo Dewji akidai alitumwa na familia ya mfanyabiashara huyo, wakati si kweli.

Katika sakata hilo, watu 7 kati ya 26 akiwemo Manara na wenzake 19 walioachwa huru kwa dhamana, bado wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam wakihusishwa na tukio la Kutekwa kwa Mo Dewji lilitokea katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam Oktoba 11 mwaka huu.

error: Content is protected !!