September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema waipa serikali fikra mpya

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani, kimeitaka serikali kuubinafsisha Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam, ili kuongeza ufanisi katika utoaji huduma. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 30 Desemba 2019 na Baraka Mwago, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani.

Mwago ameeleza kuwa, huduma zinazotolewa na mradi huo hazikidhi kiwango, na kusababisha usumbufu kwa wananchi.

Miongoni mwa adha wanayokumbana nayo watumiaji wa mradi huo, ni msongamano wa abiria vituoni na kwenye gari.

“Huu mradi wenzetu hawajajipanga. Mwendokasi wanasema wana magari 200 yamekwama bandarini lalini wanapishana na serikali kulipa kodi. Serikali ibinafsishe mradi wa mwendokasi ili wananchi wapate huduma bora,” ameshauri Mwago.

Wakati huo huo, Mwago ameishauri Serikali kukarabati miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam, ili kuondoa changamoto ya mafuriko katika jiji hilo.

Badala ya miradi hii mikubwa ambayo haina faida, fedha hii ingetumika kuikarabati miuondombinu ya Dar es Salaam. Kuboresha mifereji inayoelekea kwenye mto au baharini,” amesema Mwago.

 

error: Content is protected !!