Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema: Tunalichukua jimbo la Bukoba Vijijini
Habari za Siasa

Chadema: Tunalichukua jimbo la Bukoba Vijijini

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Bukoba Vijijini, Stanslaus Kitale
Spread the love

UONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kulichukua Jimbo la Bukoba vijijini pamoja na halmashauri kwa kushinda kata zote za udiwani. Anaripoti Danson Kaijage, Bukoba … (endelea)

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne tarehe 30 Juni 2020 na mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Bukoba Vijijini, Stanslaus Kitale alipofanya mazungumzo na MwanaHALISI ONLINE kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.

Kitale amesema, katika uchaguzi mkuu chama kinatarajia kuchukua kata zote 29 pamoja na nafasi ya ubunge ambao kwa sasa linaongozwa na Jasson Rweikiza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kitale ambaye ni Diwani wa Rubale anayemaliza muda wake amesema, wamewaandaa wagombea kwa nafasi ya ubunge na udiwani katika kata zote ambao wanauwezo mkubwa wa kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika uchaguzi huo.

Miongoni mwa waliotia nia kugombea ubunge ni Conchester Rwamlaza, Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chadema ambaye anamaliza muda wake.

Bukoba Vijijini

Katika hatua nyingine, Kitale amesema, “nimepitia katika changamoto nyingi na mimi nipo mfanyabiashara lakini nimesimama kulinda heshima yangu niliyopewa na wananchi ya kuniongoza kuwa diwani wao maana waliniamini.”

“Nimekuwa nikifuatwa na watu wa serikali pamoja na chama wakitaka nihame kwa madai ya kuunga juhudi, lakini sikufanya hivyo, nimetishiwa kafungiwa biashara lakini mimi nafanya biashara halali na ninalipa kodi zote serikalini hivyo nafanya mambo yangu katika misingi halali sikuona sababu ya kuhama,” anaeleza Kitale.

Kuhusu miradi aliyoitekeleza katika kata yake ya Rubale, amesema amefanikiwa kuwatafuta wafadhili na kuwaunganisha na jamii kwa ajili ya maendeleo.

Ameitaja baadhi ya miradi kuwa ni, ujenzi wa shule ya sekondari Rubale kutoka kidato cha nne hadi cha tano na sita, ujenzi wa mradi mkubwa wa maji, matundu tisa ya vyoo, maboma matatu ya madarasa pamoja na maabara.

Pia, matundu kumi ya vyoo katika shule ya msingi ya Nyakaju, utoaji wa ardhi kwa ajili ya upanuzi wa kituo cha polisi, ujenzi wa vyumba viwili kwa watoto wenye mahitaji maalum na ofisi ya mwalimu katika shule ya msingi Rubale.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!