Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Veta Nyamidaho-Kasulu chazinduliwa, wazazi wapewa somo
Elimu

Veta Nyamidaho-Kasulu chazinduliwa, wazazi wapewa somo

Spread the love

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Joyce Ndalichako amezindua Chuo cha Ufundi Stadi Nyamidaho kilichopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).

Chuo hicho chenye uwezo wa kudahiri wanafunzi zaidi ya 500 kimetokana na majengo yaliyokuwa yakitumiwa na Taasisi ya World Vision ambapo Serikali imekarabati majengo yaliyokuwepo na kujenga mengine mapya.

Uzinduzi huo, umefanyika jana Jumatatu tarehe 29 Juni 2020 ambapo Profesa Ndalichako alisema Sh. 534 milioni zilitolewa kwa ajili ya kazi hiyo na kwamba zimetumika Sh. 477 milioni hadi ukamilishaji.

Aidha, aliridhia ombi la kiasi kilichobaki kutumika kuanzisha ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kiume.

Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu akiangalia kifaa kilichotengenezwa katika chuo hicho

Chuo kimeanza kutoa mafunzo Februari 2020 kwa kozi nne za umeme, uashi, kompyuta na ushonaji.

Profesa Ndalichako alisema, uanzishwaji wa chuo hicho ni mwendelezo wa utekelezaji wa azma ya Serikali ya kujenga vyuo vya ufundi stadi katika kila Wilaya nchi ili kupeleka huduma hiyo karibu na wananchi na kuwapatia ujuzi vijana wa Kitanzania.

Waziri huyo, alitoa wito kwa wananchi wa maneno hayo, kuhakikisha wanawapeleka vijana wao ili kupata ujuzi na maarifa yatakayowawezesha kujipatia kipato na kuchangia katika maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Moja ya jengo la chuo hicho

Alisema katika mwaka 2019/20 vyuo 10 vya Halmashauri za Wilaya vimejengwa na kuanza kutoa mafunzo.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Emmanuel Maganga aliishukuru Wizara ya Elimu kwa kukamilisha ujenzi wa chuo hicho na kuwataka wakazi wa kijiji cha Nyamidaho kuhakikisha vijana wao hasa wa kike wanajiunga na chuo hicho.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya VETA, Peter Maduki aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuimarisha Elimu ya Ufundi nchini.

Alisema chuo hicho kipya kina wanafunzi takriban 70.

Aidha aliagiza Uongozi wa VETA kutoa bure mafunzo ya kozi ya uwashi kwa wanafunzi wanaotoka Nyamidaho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

RC Songwe ang’aka kesi 2 kati ya 60 za mafataki kuamuliwa

Spread the loveMkuu wa mkoa wa Songwe Dk. Fransis Michael ameshangazwa na...

error: Content is protected !!