MGOGORO baina ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), umemalizika baada ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kuwakutanisha viongozi wakuu wa taasisi hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)
Kikao cha viongozi hao kimefanyika leo Ijumaa tarehe 4 Septemba 2020 jijini Dar es Salam chini ya Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Wilson Mahera.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema, Dk. Ayubu Ryioba, Mkurugenzi Mkuu wa TBC na Kaimu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile.
Kila upande umeelezea kilichotokea na kwa pamoja kukubaliana kusameheana na kusonga mbele.
Msingi wa kikao hicho unatokana na Mbowe wakati wa uzinduzi wa kampeni za urais za Chadema zilizofanyika tarehe 28 Agosti 2020 Viwanja vya Zakhiem Mbagala Dar es Salaam, alitoa dakika 15 kwa waandishi wa TBC kuondoka mkutanoni hapo.
Mbowe alitoa agizo hilo akiwatuhumu kukatisha matangazo mara kwa mara wakati wakirusha moja kwa moja ‘live’ uzinduzi huo akisema, hali hiyo inawanyika fursa Watanzania kufuatilia mkutano huo.
Taarifa yote ya kilichotokea kwenye kikao hicho iliyotolewa na Katibu TEF, Neville Meena hii hapa;
Leave a comment