Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema: CCM wanatuogopa kufa, dhambi lazima waibebe
Habari za Siasa

Chadema: CCM wanatuogopa kufa, dhambi lazima waibebe

Spread the love

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amesema uamuzi wa kuzuia mikutano ya hadhara kwa kipindi cha miaka saba cha uongozi wa Rais Dk. John Magufuli haukufanywa na kiongozi huyo pekee bali pia na viongozi wa CCM hivyo dhambi hiyo lazima waibebe.

Aidha, amesema viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaiogopa Chadema kufa na wakiwaona viongiozi wa Chadema  wanatetemeka. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mbowe ametoa kauli hiyo leo tarehe 22 Januari, 2023 wakati akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa pili wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Mjini Musoma mkoani Mara.

Amesema baada ya uchaguzi wa 2015 kwa namna ambavyo Chadema waliwapelekesha mchakamchaka, CCM walikaa na kutathmini namna ya kuizuia Chadema ni kuzuia mikutano ya hadhara.

“Wakajihakikisha hawana uwezo wa kushinda uchaguzi wowote wa haki kwa hiyo njia pekee lazima watumie figisu. Yakatumika maamuzi ya ajabu.

“Nchi hii haiwezi kupata baraka za Mungu kwa sababu hatuna viongozi wenye baraka za Mungu. Utawala huu umelaanika. Uchaguzi wa 2020 hawakuiba kura, waliiba uchaguzi wenyewe.

“Hatuwezi kusema pekee CCM ni wezi bila kuwa na chama kilichojiimarisha, tunajipangaje kuleta ukombozi wa kweli katika Taifa letu,” amesema Mbowe.

Pamoja na mambo mengine ametoa wito kwa Wana-Chadema kutokubali tena Taifa lirudishwe kwenye giza la miaka saba iliyofanywa na Magufuli.

“Miaka saba ilijenga uadui kati ya jeshi la polisi na wananchi wake, kupitia maridhiano yetu tunaanza kutoka huko tunaona nuru inakuja lakini tusibweteke lazima tutafute haki yetu.

“Tumelenga kuwa na wanachama hai wenye kadi wasiopungua milioni 10, msifikiri mmeiua Chadema … pale tulipoishia ndipo tunapoanzia. Adhabu mliowapa ya kuwa utumwa kwa miaka saba mtaiona hasira yake mwaka 2025,” amesema Mbowe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

Habari za Siasa

Lissu: Miaka 30 ya vyama vingi haikupambwa kwa marumaru

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, Tundu...

error: Content is protected !!