Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Aliyekuwa msaidizi wa Rais DRC apelekwa gerezani
Kimataifa

Aliyekuwa msaidizi wa Rais DRC apelekwa gerezani

Spread the love

Fortunat Biselele, aliyekuwa msaidizi wa Rais Felix Tshisekedi wa Kongo DRC, amepelekwa katika Gereza Kuu la Makala jijini Kinshasa, baada ya malumbano ya saa sita na viongozi wa mashtaka. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Taarifa zinasema, Biselele, aliyekuwa msaidizi binafsi wa Rais Tshisekedi, alipelekwa katika Gereza hilo Ijumaa usiku tarehe 20 Januari, 2023.

Vipande vya video vimemuonesha Biselele, akisindikizwa wanajeshi kwenda katika Ofisi ya kiongozi wa mashtaka. Baadaye usiku, alionekana akiwa anasindikzwa na polisi kwenda Gerezani.

Biselele, aliondolewa kwenye Baraza la Mawaziri tarehe 14 Januari 2023,na kuzuiwa, lakini mpaka sasa hakuna sababu rasmi iliyotolewa kuhusu kukamatwa na kusimamishwa kwake kazi.

Hata hivyo, ripoti kutoka kwenye jarida la Africa Intelligence,inaeleza mshauri huyo wa zamani wa rais Tshisekedi, alikuwa anashukiwa kushirikiana na serikali ya Rais Paul Kagame nchini Rwanda.

Inaripotiwa kuwa, mwanzano mwa utawala wa Rais Tshisekedi, alijaribu kumleta karibu na Rais Kagame.

Uhusiano kati ya Kigali na Kinshasa, umeyumba, kufuatia madai ya DRC kuwa Rwanda, inawaunga mkono waasi wa M 23, shutuma ambazo rais Kagame, ameendelea kukanusha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

DCI ajitosa uchunguzi matokeo uchaguzi mkuu Kenya

Spread the loveOFISI ya Mkurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Kimataifa

Uganda yaanza kuchimba mafuta

Spread the love  UCHIMBAJI wa kwanza wa mafuta kibiashara nchini Uganda umeanza...

Kimataifa

Afrika kusini waandamana kushinikiza serikali kumaliza tatizo la umeme

Spread the love  MAMIA ya wafuasi wa Chama cha upinzani nchini Afrika...

error: Content is protected !!