Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yazindua kampeni Ushetu, yaahidi neema kwa wananchi
Habari za Siasa

CCM yazindua kampeni Ushetu, yaahidi neema kwa wananchi

Spread the love

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeanza rasmi safari ya kutetea jimbo lake la Ushetu, Mkoa wa Shinyanga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kahama … (endelea).

Ni baada ya jana Jumapili, tarehe 26 Septemba 2021, Naibu Katibu Mkuu wa CCM- Bara, Christina Mndeme kuzindua kampeni za uchaguzi huo mdogo.

CCM ambacho ni chama tawala nchini Tanzania, kimemsimamisha Emanuel Cherehani kuwa mgombea wake kwenye uchaguzo huo utakaofanyika tarehe 9 Oktoba 2021.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wake (CCM), Elias Kwandikwa kufariki dunia tarehe 2 Agosti 2021, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mwili wa Kwandikwa, aliyekuwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa ulizikwa nyumbani kwao Ushetu, tarehe 9 Agosti 2021.

Elias Kwandikwa

Akizungumza katika uzinduzi huo wa kampeni kwenye viwanja vya Nyamilangano, Christina amesema Cherehani ni mzoefu katika kutatua changamoto za wananchi wa Ushetu na walichanga karata zake ipasavyo.

“Hatukubahatisha kwa Cherehani, amekuwa kiongozi kwenye sekta zinazogusa maslahi ya wananchi wa Ushetu,” amesema Christina

Amesema, amekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa wakulima wa tumbaku, Mwenyekiti wa Chama cha mwadui na ubangwa.

Naibu katibu mkuu huyo amesema, hatua ya mgombea huyo kupewa Ilani ili kupeperusha bendera ya chama ni kumuwezesha kumsaidia kwa karibu Rais wa Tanzania, Samia Suluh Hassan ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho.

Amesema, wanatambua jukumu kubwa lililopo katika jimbo hilo, ikiwemo kumaliza changamoto za maji, barabara za kiwango cha lami, mahitaji ya wakulima wa tumbaku na  pamba.

“Naomba niwahakikishie CCM  imesikia kilio chenu katika miradi ya umeme na tayari imesitisha mkataba na mkandarasi aliyopo na tunaahidi kata 20 za jimbo hili zitafikiwa na huduma hiyo kwa haraka,” amesema

Amewaomba wananchi wa Ushetu ili kumpa heshima Rais Samia, wahakikishe hawafanyi  makosa  ifikapo tarehe 9 Oktoba 2021 kwa kumpa kura za ndiyo mgombea huyo, ili aweze kufanya naye kazi.

Naye Mgombea huyo wa Ubunge Cherehani, amesema anatambua jukumu alilonalo kwa ajili ya maendeleo ya Ushetu na anaenda kufanya kazi usiku na mchana.

“Zipo barabara ambazo ni kitovu cha maendeleo, miradi ya maji  ikiwemo wa Ziwa Victoria ni  muhimu uwe ajenda yetu, najua mama ni msikivu nami sitalala na wazembe hawatakuwa rafiki zangu,” amesema

Amesema Ilani imeelekeza na yeye anakwenda kuifanyia kazi, ikiwemo kukamilisha miradi ya afya kwakuwa jimbo hilo ni kubwa.

Amesositiza uhitaji wa soko la madini, lengo likiwa ni kuongeza mapato,  kutenga eneo la malisho kwa ajili ya wafugaji na kuongeza thamani ya zao la pamba kwa wakulima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!