Monday , 11 December 2023
Home Habari Mchanganyiko CBE kuendesha midahalo ya kitaaluma kila mwaka
Habari Mchanganyiko

CBE kuendesha midahalo ya kitaaluma kila mwaka

Spread the love

WAZIRI wa zamani wa Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Mark Mwandosya, ameishauri serikali kutunga sera ya kudhibiti matumizi ya akili bandia ili kuzuia watu kuitumia vibaya teknolojia hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Alitoa ushauri huo jana jijini Dar es Salaam, wakati wa mjadala ulioandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), na kufanyika chuoni hapo.

Profesa Mwandosya alisema bila kuwepo udhibiti wa teknolojia hiyo wanaweza kuibuka watu wakaitumia vibaya na kusababisha taharuki kwenye jamii kwa kufanya mambo ambayo hayapendezi.

Alisema teknolojia duniani inaendelea kukua kwa kasi tofauti na matarajio ya watu wengi na baadhi ya nchi wanatumia teknolojia hiyo kutengeneza vifaa kama kompyuta na magari.

“Ukiangalia kwenye viwanda vingi kwenye nchi zilizoendelea kwa sasa mashine ndizo zinafanyakazi ambazo awali zilikuwa zinafanywa na binadamu na zinafanyakazi hizo kwa haraka na kwa ubora zaidi bila matatizo,” alisema Profesa Mwandosya

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Profesa Edda Lwoga akizungumza kwenye mjadala kuhusu teknolojia duniani ulioandaliwa na chuo hicho

 “Tusipoangalia watu ambao hawawatakii mema binadamu wengine wanaweza kuitumia hiyo tekbolojia vibaya kwa hiyo naona umefika wakati wa kuwa na sera ya kudhibiti kwa sababu uzoefu unaonyesha kwamba biashara inapenda sana kushamiri ambako hakuna sera wala udhibiti, “ alisema

Profesa Mwandosya ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA), alisema sasa hivi dunia inaondokana na  magari yanayotumia mafuta ambayo yamekuwa yakizalisha hewa ya ukaa unaosababisha joto duniani.

Alisema wazalishaji wa magari wanaondokana na teknolojia ya magari ya sasa yanayotumia petrol na dizeli na kwenda kwenye matumizi ya betri za umeme na wameshaanza kuyatengeneza.

Washiriki wa mjadala ulioandaliwa na CBE wakifuatilia

“Bila shaka nasisi Tanzania tutakuwa tumeliona hilo kwa hiyo kwa upande wetu tunapaswa kuanza kutengeneza sera ya matumizi ya magari ya umeme, nimesisitiza hilo kwa sababu Tanzania tumegundua madini ambayo yatatengeneza betri zinazotumika kwenye magari ya umeme,” alisema

Alisema kuna nchi duniani zimegundua teknolojia ambapo mtu anaweza kuchaji betri kwa dakika kumi na kusafiri na gari lake kutoka jijini Dar es Salaam hadi mkoani Mbeya bila kulazimika kuchaji tena.

“Lazima tufanye kitu tusingoje teknolojia itukute wakati hatujajitayarisha tunaweza kuwa kwenye matatizo kwa hiyo lazima wataalamu tuishauri serikali kuja na sera itakayolisaidia taifa tusije kujikuta tunaishi kwenye karne iliyopita,” alisema

Naye Mkurugenzi wa Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Dk. Nkundwe Mwasaga, alisema  teknolojia inatakiwa kuongeza ubunifu na kuchochea shughuli mbalimbali za kiuchumi.

“Sisi tume tunasimamia masuala ya mapinduzi ya kidijitali na kwenye mapinduzi hayo tunaangalia nguzo tano, moja ya nguzo hizo ni kuongeza ujuzi wa watanzania, kuhakikisha mifumo inakuwa salama na inawezakuaminina, kuhakikisha huduma za mawasiliano  zinapatikana maeneo yote bila ubaguzi wowote, kutengeneza uchumi wa kidijitali unaojumuisha watanzania wote na kuhakikisha masuala ya utafii ubunifu na ujasiriamali wa kidijitali unatumiwa vizuri ili tuwe na kampuni nyingi za kisasa,” alisema

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Profesa Edda Lwoga akizungumza kwenye mjadala kuhusu teknolojia duniani ulioandaliwa na chuo hicho

Mkuu wa chuo cha CBE, Profesa Edda Lwoga, alisema chuo hicho kimekuwa kikiandaa midahalo kama hiyo mara kwa mara ambayo inatoa suluhisho kwa changamoto kwa kutoa mawazo mbadala.

“Tumeamua tuwe na midahalo kama hii kwasababu sisi wajibu wetu ni kutoa taaluma, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu sasa kama tutafanya tafiti na kuzifungia tu kwenya makabati hatutkuwa tunasaidia taifa letu kwa hiyo tukaona midahalo hii ya mtandaoni kama sehemu ya kutoa taarifa,” alisema Profesa Lwoga

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kesi ya mfanyakazi wa CRDB itaendelea J’tatu

Spread the love  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam inatarajia...

Habari Mchanganyiko

Mawasiliano Dar – Bagamoyo yarejea

Spread the loveMAWASILIANO ya barabara ya Mkoa wa Pwani na Dar es...

Habari Mchanganyiko

Tanesco: Mvua chanzo kukatika umeme leo

Spread the loveShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limedai kuwa hitilafu iliyojitokeza katika...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Zara tours yajivunia kupandisha wageni 228 Mlima Kilimanjaro

Spread the loveKampuni ya utalii ya Zara tours ya mjini Moshi mkoani...

error: Content is protected !!