Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge laazimia kumsulubu Makonda
Habari za SiasaTangulizi

Bunge laazimia kumsulubu Makonda

Bunge la Tanzania. Picha ndogo Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Spread the love

WAKATI Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiendesha kampeni yake ya dawa za kulevya jijini Dar es Salaam, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepanga ‘kumsulubu,’ anaandika Faki Sosi.

Taarifa kutoka mjini Dodoma zinaeleza kuwa, tayari bunge hilo limempeleka Makonda mbele ya Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge.

Ofisi ya Katibu wa Bunge imeagizwa wamtake Makonda apeleke maelezo kutokana na kutuhumiwa kutoa kauli ya kulidharau bunge.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya wabunge kulalamika kwamba, Makonda amekuwa akidharau muhimili huo.

Bunge liliibua tuhuma kwa Makonda kutokana na mali anazozimiliki huku wakitaka kujua chanzo chake.

Baada ya kuibuliwa tuhuma hizo bungeni, mbele ya waandishi wa habari Makonda alisema kwamba, wakati mwingine watunga sheria hao (wabunge) hulala bungeni kwa kukosa cha kuzungumza.

Kauli hiyo iliibua hasira kwa wabunge hao miongoni mwao akiwa Abdallah Ulega, Mbunge wa Jimbo la Mkuranga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Jana bungeni Ulega amesema “…siku alipokuja kipenzi chetu Dk. Magufuli (Rais John Magufuli) na kuhutubia bunge hili, tulimshangilia kwa nguvu alipotangaza vita dhidi ya dawa za kulevya.

“Leo wabunge wanaambiwa hawana jambo la kuzungumza isipokuwa wanafanya kazi ya kulala kwenye bunge hili,” amesema Ulega ambaye pia ni Naibu Katibu wa Wabunge wa CCM.

Amesema kuwa, jana walipata kauli ya Makonda kupitia vyombo vya habari na kwamba, kwa namna moja ama nyingine zinaonesha dhahiri kulidharau bunge.

Hata hivyo Ulega amesema kuwa, wabunge wapo mstari wa mbele kuhakikisha wanapambana na kumsaidia Rais Magufuli katika vita dhidi ya dawa za kulevya na kuwa, sheria inayosimamia vita hivyo imetungwa na bunge.

Wakati akitoa kauli hizo Ulega alikuwa akishangiliwa na wabunge kwa kupigiwa makofi “kuna mawili; ama huyu kijana mwenzangu hakuwa anajua anachokisema au amefanya dharau ya makusudi.”

Ulega amelieleza bunge kwa kumwomba Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu ambaye ndio kiongozi mkuu wa shughuli za serikali kuchukua hatua za makusudi kulinda heshima ya bunge.

Pia bunge litumie kanuni zake kupitia kanuni ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ili kuchukua hatua stahiki za kulinda bunge hilo dhidi ya Makonda.

Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini ameungana na Ulega kwa kutaka kuhakikisha kanuni za bunge zinatumika vilivyo ili kukabiliana na wale wanaotaka kupuuza ama kuudharau muhimili huo.

Andrew Chenge, Mwenyekiti wa Bunge ambaye alikuwa kwenye kiti jana ameeleza kuwa, “kitu chochote ambacho kina tabia au kudaharau na kushusha hadhi ya bunge hili, hakikubaliki hata kidogo.”

Pia Chenge mesema, “naagiza Ofisi ya Katibu wa Bunge, kwa taratibu zilizopo, wamtake Makonda alete maelezo kama amesema kweli na yapelekwe Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!