August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lissu agoma kula, ashinikiza kupelekwa mahakamani

Wakili Peter KIbatala (kushoto) akijadili jambo na mteja wake, Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki

Spread the love

TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, amegoma kula chakula kutwa nzima ya leo, akishinikiza kupeleka mahakamani, anaandika Faki Sosi.

Kwa mujibu wa wakili wa Lissu, Peter Kibatala, mteja wake amegoma kula toka asubuhi, mchana na jioni kwa madai hata fanya hivyo mpaka atakapopelekwa mahakamani.

“Mke wa Lissu alileta chakula asubuhi, lakini Lissu aligoma kula na kumwambia mkewe asihangaike kwani hatakuka mpaka atakapofikishwa mahakamani,” amesema Kibatala.

Kibatala amesema kwa sasa wanapigania mteja wake apelekwe mahakamani kwani muda wa kisheria kushikiriwa kituoni umemalizika.

Lissu alikamatwa jijini Dodoma nje ya viwanja vya Bunge, Februari 6, 2017 na kuletwa Dar es Salaam katika kituo cha Polisi cha Kati kwa mahojiano, huku kosa lake likidaiwa ni kauli za uchochezi.

error: Content is protected !!