Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara ‘Bonge la Mpango’ ya NMB yafikia tamati, wateja wajishindia zawadi nono
Biashara

‘Bonge la Mpango’ ya NMB yafikia tamati, wateja wajishindia zawadi nono

Spread the love

KAMPENI ya uhamasishaji wa kuweka akiba ya Benki ya NMB iliyopewa jina la ‘Bonge la Mpango’ Msimu wa Tatu imefikia kilele tarehe 5 Julai 2023 na kuwafanya wateja wenye bahati kushinda zawadi nono zenye thamani ya Sh 69.5 milioni.

Wateja hao wamejishindia zawadi katika droo kubwa ya kampeni hiyo iliyofanyika kwenye banda la benki hiyo katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Zawadi zilizoshindwa ni pamoja na bajaji za mizigo tano zenye thamani ya Sh. 25 milioni, pikipiki 11 zenye thamani ya Sh 33 milioni, friji (jokofu) la kisasa la milango miwili, Smart Tv, mashine ya kufulia nguo, Laptop, simu ya Samsung Z Flip pamoja na simu ya iphone 14 ProMax.

Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Matawi wa Benki ya NMB, Donatus Richard (katikati),  akionesha sehemu ya zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa Droo ya mwisho ya Bonge la Mpango – Moto Uleule iliyofanyika kwenye viwanja vya Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam tarehe 5 Julai 2023. Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper na kulia ni Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Ibrahim Sikana

Akizungumza wakati wa kuchezesha droo hiyo, Mkuu wa Mtandao wa Matawi na Mauzo ya Rejareja wa Benki ya NMB, Donatus Richard alisema kampeni ya benki hiyo ilikuwa na lengo la kuhamasisha uwekaji wa akiba na ililenga kukuza utamaduni wa kuweka akiba kwa wateja wake.

“Tulikuja na kampeni hii ambayo kwa namna moja au nyingine imesaidia idadi kubwa ya wateja wetu kuwa na tabia ya kujiwekea akiba ili wasipate wakati mgumu wanapokumbana na masuala yenye udharura,” alisema Richard.

Richard alisema katika droo za awali za kampeni hiyo, benki yake ilitoa zawadi za Sh. 110 milioni kwa wateja wake 178 wakati wa kampeni hiyo iliyozinduliwa tarehe 29 Machi 2023.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper, akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya mwisho ya  Bonge la Mpango – Moto Uleule iliyofanyika kwenye viwanja vya Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam tarehe 5 Julai 2023.

“Ili kurudisha faida tunayoipata kama benki kwa wateja wetu, tulizindua promosheni hii tarehe 29 Machi na tumeshuhudia zawadi za pesa taslimu, vifaa mbalimbali vya kielektroniki zikiwemo friji, TV, pikipiki huku zawadi za pesa zikiwekwa katika akaunti za washindi, lengo likiwa    kuhamasisha wateja kuendelea kuwa na akiba katika akaunti zao,” alisema Richard.

Aliongeza kuwa benki hiyo inatambua kuwa uwekaji wa akiba kwa watanzania ni jambo gumu kidogo kwani wengi wao hushindwa kutunza pesa iliziweze kuwasaidia baadae na badala yake  hulazimika kukopa mikopo tena kwa riba kubwa.

Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Matawi wa Benki ya NMB, Donatus Richard (kushoto),  akibonyeza kitufe cha kompyuta kumtafuta mmoja wa washindi wa Droo ya mwisho ya Bonge la Mpango – Moto Uleule iliyofanyika kwenye viwanja vya Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam tarehe 5 Julai 2023. Kulia ni Meneja Mauzo wa NMB, Janeth Nyamko na wa pili kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper.

Richard alisema kuwa kutokana na hilo, NMB imejidhatiti kuendelea kuhamasisha matumizi ya akaunti za NMB kwa wateja wake kama njia ya kuhifadhia fedha  na kujiwekea akiba.

Katika hafla hiyo, Mwakilishi wa Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, Ibrahim Sakina aliipongeza benki hiyo kwa kuzindua kampeni ambayo siyo tu inahamasisha uwekaji akiba, bali pia inaongeza matumizi ya fedha kupitia mifumo rasmi.

“Sisi kama bodi, tunaipongeza benki ya NMB kwa kuanzisha kampeni hii. Katika droo ya leo, kumekuwepo na uwazi wa hali ya juu na washindi wote wamepatikana kihalali,” alisema.

Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Matawi wa Benki ya NMB, Donatus Richard (wa pili kushoto),  akipiga makofi baada ya kumpata  mmoja wa washindi wa Droo kubwa ya  mwisho ya Bonge la Mpango – Moto Uleule iliyofanyika kwenye viwanja vya Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam tarehe 5 Julai 2023. Wa pili kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper, Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Ibrahim Sikana (kushoto) na kulia ni Meneja Mauzo wa NMB, Janeth Nyamko.

Washindi wa zawadi za promosheni ya ‘Bonge la Mpango’ Msimu wa Tatu ya  Benki ya NMB wanatarajiwa kukabidhiwa zawadi zao  Ijumaa wiki hii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

error: Content is protected !!