Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Biashara Benki ya Exim yafuturisha wateja wake Tanga
Biashara

Benki ya Exim yafuturisha wateja wake Tanga

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashimu Mgandilwa akizungumza na wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wateja wake jijini Tanga.
Spread the love

IKIWA ni muendelezo wa utaratibu wake wa kuandaa futari kwa ajili ya wateja na wadau wake katika mikoa mbalimbali nchini kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Benki ya EximTanzania mwishoni mwa wiki iliandaa futari maalum kwa ajili ya wateja wake mkoani Tanga. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashimu Mgandilwa (kulia) akipata futari sambamba na maofisa waandamizi wa benki ya Exim akiwemo Mkuu wa idara ya wateja wadogo na kati Benki ya Exim, Andrew Lyimo (wa pili kushoto), Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo, Stanley Kafu (Kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa huo Sheikh Juma Luwuchu (wa pili kulia) wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wateja wake jijini Tanga mwishoni mwa wiki.

Hafla ya futari hiyo ilifanyika Hotel ya Tanga Beach Resort jijiji Tanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo wateja, wafanyakazi wa benki hiyo.

Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Tanga, Ibrahim Ukwaju akizungumza na wageni waalikwa waliohudhulia hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wateja wake jijini Tanga ikiwa ni muendelezo wa utaratibu wa benki hiyo wa kuandaa futari kwa ajili ya wateja na wadau wake katika mikoa mbalimbali nchini kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Hafla hiyo ilifanyika Hotel ya Tanga Beach Resort jijiji Tanga mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo wateja, wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali.

Pia viongozi mbalimbali wa serikali walihudhuria wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashimu Mgandilwa pamoja na Sheikh Mkuu wa Mkoa huo, Juma Luwuchu.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Juma Luwuchu akizungumza na wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wateja wake jijini Tanga.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari

Bosi utalii atoa ujumbe wa mikopo nafuu ya NMB

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini...

BiasharaHabari

NMB yavutia wabunifu suluhisho za kifedha, Dk. Mpango agusia vijana

Spread the love  MFUMO wa majaribio wa suluhishi za kifedha ulioandaliwa na...

BiasharaHabari

NMB Nuru Yangu yazinduliwa, 200 kunufaika

Spread the loveBENKI ya NMB nchini Tanzania imetangaza rasmi kuanza kupokea maombi...

BiasharaHabari

Waziri Bashe uso kwa uso vigogo NMB bungeni

Spread the loveWAZIRI wa Kilimo nchini Tanzania, Hussein Bashe amekutana na kufanya...

error: Content is protected !!