Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge viti maalum CCM afariki
Habari za SiasaMpya

Mbunge viti maalum CCM afariki

Spread the love

 

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Tulia Ackson ametangaza kifo cha Mbunge wa Viti Maalum,CCM, Irene Alex Ndyamkama ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma …  (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Aprili 24,2022 na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa Ofisi ya Bunge jijini Dodoma imeeleza kuwa, Ndyamkama amefariki leo Aprili 24,2022 katika Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoani Pwani wakati akipatiwa matibabu.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mheshimiwa Irene Alex Ndyamkama, Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wabunge na wananchi wa Mkoa wa Rukwa. Mwenyenzi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,”amesema Spika.

Aidha, Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!