September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Maandalizi sensa ya watu na makazi yamekamilika kwa asilimia 80

Spread the love

SERIKALI imesema Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti mwaka huu yamefikia hatua ya asilimia 80. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Pia imesema sensa ya mwaka huu itafanyika kidigitali hivyo itakuwa mfano kwa nchi nyingi za Afrika kuja kujifunza namna ya kuendesha zoezi hilo.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 24 Aprili, 2022 jijini Dodoma na Kamishina wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Spika Mstaafu Anne Makinda wakati akifungua Mafunzo ya Waratibu wa Sensa ngazi ya mkoa na wilaya.

Makinda amewataka waratibu hao kuhakikisha wanatanguliza uzalendo katika kufanikisha zoezi hilo hasa kipindi cha kuchangua makarani na wasimamizi wa zoezi hilo.

“Ni marufuku kuweka undugu katika zoezi la kutafuta makarani na wasimamizi wa sensa ni vyema mkatanguliza uzalendo pia kuna vifaa vya sensa mtakavyopewa mkavitunze na baada ya zoezi kumalizika virejeshwe mahali husika. Haitaleta picha nzuri kuona mtu anapewa vifaa anatumia hivyo hivyo mwisho wa siku vinapotea au kuharibika,” amesisitiza.

Naye Mtakwimu Mkuu wa Serikali Tanzania Bara, Dk. Albina Chuwa amesema mandalizi ya sensa ya watu na makazi yamefikia asilimia 80 bado asilimia 20 ambazo hadi kufikia Agosti 23 mwaka huu siku ya sensa yatakuwa yamekamilika kwa asilimia 100.

Aidha, Dk. Chuwa amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuhakikisha sensa ya watu na makazi ya mwaka huu inafanyika kipekee kwa sababu itaunganisha sensa ya majengo na watu.

“Kazi kubwa iliyobakia ni kupata mwongozo ikiwemo kupata makarani na wasimamizi wa sensa na mafunzo yataanza Juni 2 mwaka huu kwa ngazi ya Taifa kwa ngazi ya Taifa na Julai itaanza ngazi ya Mkoa,” amesema.

Ameongeza kuwa:” Kila mmoja awe makini kupokea kitakachowasilishwa na kutoa ushauri chanya lengo ni kuhakikisha watu wote wanahesabiwa kwa mara moja usiku wa kuamkia siku ya sensa na miongozo itatokewa ili kuhakikisha kila kundi linafikiwa.

“Sensa ya mwaka huu itakuwa ya kipekee sensa na itafanyika kidijitali tunataka Tanzania iwe kitovu cha nchi nyingine za Afrika waje hapa kujifunza namna ya kutekeleza zoezi hili,” amesema.

Aidha, Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022- Zanzibar, Balozi Mohmed Haji Hamza ametoa wito kwa makarani na wasimamizi watakaopewa jukumua la kusimamia zoezi hilo kuhakikisha wanatekeleza wa ufanisi na kuhakikisha elimu na uhamasishaji unawafikia wananchi wote.

Awali Mwakilishi wa Mtakwimu Mkuu Wa Zanzibar, Abdulmajid Jecha amesema ni vyema wasimamizi wa sensa kuhesabu mara moja tu watu wote watakaolala nchini kuamkia siku ya sensa.

Mafunzo hayo kwa waratibu wa sensa ngazi ya moa na wilaya yatafanyika kwa siku mbili ambayo lengo la mafunzo hayo ni kutafakari ushindi wa asilimia 100 wa utekelezaji zoezi la sensa ya watu na makazi.

error: Content is protected !!