October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bashange ataka ukatibu mkuu ACT-Wazalendo

Spread the love

JORAM Bashange, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi na Kampeni ya Chama cha ACT-Wazalendo, amechukua fomu ya kugombea nafasi ya katibu mkuu kwenye chama hicho. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Leo tarehe 10 Februari 2020, Bashange amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo kwenye Makao Makuu ya chama hicho, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuchukua fomu hiyo, Bashange amesema kuwa amejipima na kufanya tafakuri binafsi, na kuona anatosha kwenye nafasi hiyo.

“Nimesoma Katiba na kuona majukumu yake, nimeangalia kanuni za kudumu za uendeshaji wa chama na kufanya tafakuri binafsi na kuona, kwamba nafasi hii inanitosha kuitumikia,” amesema.

Uchukuaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali za chama hicho, ulianza tarehe 27 Januari 2020, na utakamilika tarehe 26 Februari 2020.

error: Content is protected !!