December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Balozi Mahiga awatwisha mzigo maofisa wake

Balozi Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria

Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga amewahimiza maafisa wa wizara yake waliopo nje ya nchi kutafuta wawekezaji, ili waje kuwekeza Tanzania. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Balzi Mahiga ametoa agizo hili katika hafla za uzinduzi wa hati za kusafiria na vibali vya ukaazi kwa njia ya kielektroniki (E-VISA & E-PERMIT), ambapo amewataka maafisa hao kujitahidi katika hilo ili kusaidia jitihada za serikali za kufikia uchumi wa viwanda.

Kuhusu uzinduzi wa visa na vibali vya ukaazi kwa njia ya kielektroniki, Balozi Mahiga amesema mfumo huo mpya utarahisisha Tanzania kupata wawekezaji wengi.

Balozi Mahiga ameagiza utaratibu wa ukaguzi wa wageni wanaoingia nchini hasa watalii ufanyike kwa njia rafiki ili kuondoa malalamiko.

error: Content is protected !!