February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Zitto Kabwe yaiva

Zitto Kabwe akitinga mahakamani Kisutu

Spread the love

UPANDE wa Mashtaka katika mashauri matatu ya uchochezi yanayomkabili Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, umekamilisha upelelezi wa mashauri hayo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi leo tarehe 26 Novemba 2018 mbele ya Hakimu, Huruma Shahidi amedai kwamba upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

Baada ya maelezo hayo ya upande wa mashtaka, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga tarehe 13 Desemba mwaka huu kuwa siku ya kumsomea maelezo ya awali (PH), Zitto.

Upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Peter Kibatala ulidai kuwa hauna pingamizi juu ya tarehe hiyo.

Zitto anadaiwa kutenda makosa hayo tarehe 28 Oktoba 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!