March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Babu Seya atinga Ikulu kumshukuru Rais Magufuli

Mwanamuziki Nguza Vicking “Babu Seya” na wanae Johnson Nguza “Papii Kocha”, Francis Nguza na Michael Nguza wakiwasili Ikulu

Spread the love

Mwanamuziki Nguza Vicking “Babu Seya” na wanae Johnson Nguza “Papii Kocha” Francis Nguza na Michael Nguza leo wamefika Ikulu kumshukuru Rais wa Tanzania, John Magufuli kwa msamaha aliotoa kwao dhidi ya kifungo cha maisha walichokuwa wakitumikia gerezani, anaandika Hamis Mguta.

Rais Magufuli alitoa msamaha huo Disemba 9 mwaka jana, akiwa Dodoma katika sherehe za miaka 56 ya Uhuru.

Mwaka 2003, Babu Seya na wanaye watatu walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kubaka na kulawiti watoto wa Shule ya Msingi Mashujaa ambapo mwaka 2004, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar iliwahukumu wote wanne kifungo cha maisha jela.

Baada ya hukumu hiyo, walikata rufaa lakini mwaka 2005, Mahakama Kuu iliridhia hukumu hiyo ya kifungo cha maisha jela kwa wote wanne kabla ya Mahakama ya Rufaa kuwaachia huru watoto wawili wa Nguza – Mbangu “Nguza Mashine” na Francis  Nguza “Chichi” mnamo Februari 2010.

Nguza amesema “Muheshimiwa rais alinisamehe kule, nimekuja kutoa shukrani zangu za dhati kutoka ndani ya moyo wangu na kumuomba aniruhusu sasa kuanza kufanya kazi.

“Kuanzia sasa nipo huru kufanya kazi, mashabiki wanipe muda kidogo nitawatangazia lini nitanza kuingia jukwaani.”

 

error: Content is protected !!