MBUNGE wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na mratibu wa chama hicho Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wameitwa Polisi. Anaripoti Hamisi Mguta … (endelea).
Wawili hao wamesema hawajui sababu ya wito huo huku wakisema kuwa wanahisi wito huo unatokana na mkutano wa hadhara alioitisha Sugu katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
Sugu amesema juzi jioni alipigiwa simu na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya (RCO) kwamba wafike jana ofisini kwake kuzungumza lakini alimueleza ilikuwa ni siku ya sikukuu hivyo itakuwa ngumu kwenda na wakakubaliana walikubaliana wafike leo.
“Walinipigia simu juzi jioni wakinitaka mimi na Masonga twende makao makuu ya polisi jana, nikawaambia itakuwa ni sikukuu hivyo tukakubaliana leo asubuhi, hivyo tupo njiani tunaelekea huko kuitika wito. Sijajua sababu, lakini nadhani ni uchochezi,” amesema Sugu.
Katika mkutano huo unaodhaniwa kuwa ndio chanzo, Masonga ndiye aliyemkaribisha Sugu kuzungumza na wananchi na alifunga mkutano, lakini kabla ya kumkaribisha alizungumza machache kuhusu mustakabali wa Taifa.
Leave a comment