March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TCRA yaihukumu Azam TV, Star TV

Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Joseph Mapunda

Spread the love

MAMLAKA ya mawasiliono nchini TCRA imetoa hukumu kwa televisheni nne kwa tuhuma za uchochezi  na kukiuka  kanunuzi za utangazaji, Anaripoti Faki Sosi….(endelea)

Mamlaka hiyo kupitia timu yake ya kamati ya maudhui  imevipa adhabu ya kulipa faini  kituo cha televisheni  Star tv, Azam tv Channel ten pamoja na East Africa Tv.

Akisoma hukumu hiyo  hiyo Makamo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Joseph Mapunda amesema kuwa vituo hivyo vimefanya uchochozi kwa kutangaza habari ya kituo cha sheria na  haki za binaadamu kilipokuwa klikitoa tathimini ya uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 uliofanyika  Novemba 30 mwaka 2017 sehemu mbalimbali nchini.

Taarifa ya Kituo cha sheria na haki za binadamu ileelza kuwa  waangalizi wa kituo hicho walifika sehemu mbalimbali zilizofanyika uchaguzi huo na kubaini uvunjwaji wa haki za binadamu, utekwaji na upigwaji wa watu umejitokeza kwenye uchaguzi huo na kwamba vitendo hivyo vimetekelezwa na vyomvo vya dola pamoja na wafuasi wa vyama mbalimbali  vya siasa.

Mapunda ameendelea kusema kuwa vyombo hivyo vilitangaza taarifa hizo bila kuthibitisha ukweli wa taarifa hiyo kwa kuzungumza na wahusika wa wa mamlaka zilizotuhumiwa kama vile Tume ya uchaguzi  NEC au jeshi la Polisi.

Amesema kuwa vyombo hivyo vimepewa adhabu hiyo kutokana kukiuka kanuni za utangazaji , kutangaza habari za uchochezi zingeweza kuhatarisha usalama wa taifa, kutangaza habari ambazo hazikutibitishwa ukweli wake pamoja na  kushindwa kufanya mizania

Hivyo vituo hivyo vimepewa adhabu  ya kulipa faini, vituo hivyo  ni pamoja na  azamu kulipa shilingi 7.5 milioni,  Star tv Shilingi  7.5 milioni na East Afrika tv Shilingi Mil 15milioni pamoja na channel ten 15 milioni.

Mapunda amesema kuwa faini hiyo italipwa ndani ya siku 30 kuanzia leo tarehe 2 januari licha kuwepo wazi kwa rufaa kwa wamiliki wa vyombo hivyo kwa muda wa siku 30 pamoja na kuwekwa chini ya uangalizi kwa muda wa miezi sita kuanzia sasa.

 

error: Content is protected !!