Monday , 4 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha
Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Loy Thomas Sabaya
Spread the love

Loy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameshinda nafasi ya Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Ushindi huo umekuja baada ya Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichoketi wiki iliyopita pamoja na mambo mengine, kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya chama kwa ngazi ya mkoa na wilaya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali.

Kupitia uchaguzi huo uliofanyika Ukumbi wa AICC jijini Arusha, Loy Thomas Sabaya ameshinda kwa kupata kura 463 kati ya kura 907 zilizopigwa katika nafasi ya mwenyekiti.

Dk. Daniel Mrisho Pallangyo amepata kura 374, Solomoni Olesendeka Kivuyo amepata kura 59,Edna Israel Kivuyo amepata kura 10 na kura moja ikaharibika.

Lengai Ole Sabaya

Uchaguzi huo uliosimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka, umefanyika baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Zelothe Stephen kufariki dunia tarehe 26 Oktoba 2023.

Zelothe alifariki alipokuwa jijini Dar es Salaam, alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwinyi aungana na Samia kuuaga mwili wa baba yake

Spread the loveRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mtoto wa Mzee Mwinyi amwaga machozi

Spread the loveMtoto wa Hayati mzee Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi ameshindwa...

Habari za SiasaTangulizi

Mzee mwinyi alikuwa mwanademokrasia wa kweli

Spread the loveMtoto wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Mwinyi alikuwa maktaba inayotembea

Spread the loveRais Samia Suluhu hassan amesema Hayati rais mstaafu, Ali Hassan...

error: Content is protected !!