Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko RPC Songwe awafunda trafki kuzingatia uadilifu
Habari Mchanganyiko

RPC Songwe awafunda trafki kuzingatia uadilifu

RPC Songwe
Spread the love

ASKARI wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Songwe wametakiwa kuendelea kufanyakazi kwa kuzingatia haki, weledi na uadilifu hatua ambayo itachangia kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani ambavyo vimekuwa vikisababisha ajali. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa jana Jumapili na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Theopista Mallya wakati alipokutana na kuzungumza na askari hao.

Aliwataka kuchukua hatua kwa yeyote atakayebainika kufanya vitendo visivyokubalika kisheria hasa kwa watumiaji wa vyombo vya moto wawapo barabarani.

Kamanda Mallya aliwasisitiza na kuwataka askari hao kufanya kazi kwa kusimamia sheria, kanuni na taratibu na kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia uadilifu na kutenda haki ili kuleta matokeo chanya.

Sambamba na hayo, pia alikemea mambo kadha wa kadha ikiwemo kuacha vitendo vya kujihusisha na rushwa sambamba na vitendo  vingine ambavyo vinaweza kuharibu taswira ya Jeshi la Polisi.

Kamanda Mallya alitumia kikao kazi hicho kwa kutoa wito kwa wananchi hasa wale wanaotumia vyombo vya moto na hata watembea kwa miguu kufuata kanuni, sheria na alama za barabarani na pia kuwaripoti madereva wanaovunja sheria ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!