August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

AWA watamba kupunguza majangili wa Tembo

Tembo

Spread the love

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyama Pori (TAWA), imesema kwamba tatizo la ujangili katika mbuga mbalimbali umepungua hatua iliyosababisha Tembo kuongezeka, anaandika Dany Tibason.

Hatua hiyo imetokana na kutolewa elimu mbalimbali kuhusu umuhimu wa wanyama hao kwa nchi pamoja na kuimarisha vikosi vya ulinzi.

Hayo yamesemwa na Ofisa Habari na Mahusiano wa mamlaka hiyo, lielezwa na Afisa habari na Mahusiano wa Mamlaka hiyo, Twaha Twaibu alipozungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya maonesho ya kilimo na mifugo katika manispaa ya Dodoma.

“Tumeboresha zaidi mazingira ya maonesho ya nane nane kwa sasa tumeleta wanyama tofauti na miaka mingine kwa sasa tumeleta, Mamba,Tusi ambao wanaonekana zaidi Ikulu, Nyati, Ndege aina aina ya Taji Korongo wanaotumika katika nembo ya bendera ya nchini Uganga,”

error: Content is protected !!