Saturday , 2 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Meya wa Chadema amvaa Rais Magufuli
Habari za SiasaTangulizi

Meya wa Chadema amvaa Rais Magufuli

Boniface Jacob, Meya wa Manispaa ya Ubungo. Picha ndogo Rais John Magufuli.
Spread the love

BONIPHACE Jacob, Meya wa Manispaa ya Ubungo amewalalamikia watendaji wa Rais John Magufuli kwa kuwa wanakwamisha miradi ya maendeleo katika maeneo ambayo yanaongozwa na upinzani, anaandika Hellen Sisya.

Meya huyo amepinga kauli ya Rais Magufuli kwamba serikali haibagui chama wakati serikali inapofanya maendeleo ya wananchi, kwa kuwa Ubungo na Kibamba wanabaguliwa.

Manispaa ya Ubungo inaundwa na Majimbo mawili ya Ubungo ambalo linaongezwa na Mbunge, Saed Kubeneo (Chadema) na Kibamba linawakilishwa na John Mnyika (Chadema).

Akihutubia mkutano wa hadhara uliondaliwa na Mbunge Kubenea, Meya huyo alisema, kuna ubaguzi mwingi unafanywa na serikali kwa kigezo za itikadi za vyama.

Akiwa katika eneo la Kimara Kilungule lililopo katika jimbo la Ubungo, Meya huyo amesema kuwa kauli ya Rais Magufuli kwamba serikali haibagui chama katika kufikisha maendeleo kwa wananchi siyo ya kweli.

Meya huyo alisema kuwa, serikali kupitia kwa Dotto James, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mmipango, imeizuia fedha zilizotolewa na Benki ya Dunia (WB),kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika jiji la Dar es Salaam ambalo linaongozwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)

“Wapinzani baada ya kuchukua halmashauri za jiji la Dar es salaam, WB ilituzawadia kiasi cha Sh. billion 600 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Tangu mwaka 2015 fedha hizo zimezuiwa ambazo zingesaidia kuharakisha maendeleo katika jiji la Dar es salaam,” amesema

Aidha, Meya huyo amesema kuwa wakati akiongoza Manispaa ya Kinondoni, serikali ilihujumu ujenzi wa kiwanda cha taka cha mbolea ambacho kilipaswa kujengwa katika eneo la Mabwepande kwa msaada wa Wajerumani.

Meya huyo ameongeza kuwa serikali kupitia kwa Dotto James ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika wizara hiyo hiyo, aliwaandikia Wajerumani waliotoa fedha hizo na kuwataka walipe kodi kwa ajili ya mitambo.

Amesema baada ya kutolewa agizo hilo, wafadhili walikataa na hivyo kurudisha mitambo yao ambayo wangeitumia kujenga kiwanda.

Aidha, amesema baada ya kuhamia Manispaa ya Ubungo, Meya wa Kinondoni ambaye anatoka katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliwaandikia Wajerumani barua ya kuwaomba walete mitambo yao jambo ambalo walilikataa.

“Baada ya mimi kuondoka Kinondoni nimekuja Ubungo, meya wa Kinondoni wa CCM, aliwaandikia wajerumani barua kwamba sasa hivi hakuna shida leteni huo mtambo. Wajerumani wamenitumia ile barua ya Kinondoni ya CCM, kwamba wamekunyima wewe, sasa umeondoka wanataka tulete mtambo. Na wazungu wamenionesha majibu wamewajibu kwamba hatuleti tena, muda haupo” alisisitiza Boniphace

Aidha, meya huyo alitoa wito kwa wakazi wa jiji hilo kupaza sauti zao popote walipo ili serikali iweze kuachia fedha ambazo zilitolewa na WB kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari za Siasa

Rais Samia kuzindua programu ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua programu ya...

Habari za Siasa

AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili

Spread the loveMWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, ameagiza Kamati...

Habari za Siasa

Jaji avunja ukimya sakata la Mpoki kusimamishwa uwakili

Spread the loveJAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amekitaka Chama cha...

error: Content is protected !!