
Wafanyakazi wa Manji wakiingia mahakamani
MFANYABIASHARA Yusuf Manji na wenzake watatu wamezidi kusota rumande baada ya kesi yake kupigwa kalenda hadi Agost 9, mwaka huu, anaandika Faki Sosi.
Kesi hiyo ipo mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu, Huruma Shahidi na Wakili wa serikali Kisenyi Mutalemwa, aliomba tarehe nyingine ya kuitaja kwa kuwa ushahidi haujakamilika.
Manji na wenzake walifikishwa kizimbani kwa tuhuma za kukutwa na sare jeshi pamoja na tuhuma nyingine zinazohusu masuala ya usalama wa nchi.
More Stories
Askofu Kilaini alaani Klabu ya Simba kutumia msalaba kwa dhihaka
NMB kunufaisha sekta ya kilimo Tanzania
Dk. Mwinyi: Utafiti ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa