December 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Askofu Gwajima aeleza kiini cha nchi kukwama

Askofu Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe

Spread the love

 

ASKOFU Josephat Gwaji, Mbunge wa Kawe, Dar es Salaam amesema, Afrika ikiwemo Tanzania haziwezi kuendelea kwa kuwa, hazina utaratibu wa kuendeleza agenda za awamu zilizopita. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Amesema, ili Tanzania ipige hatua, inahitajika mjadala wa kitaifa sambamba na kutafsiri maana ya maendeleo kwa miaka 30 au 50.

Askofu Gwajima ametoa kauli hiyo leo tarehe 15 Aprili 2021, wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2021/22.

“Ili tuendelee tunahitaji ajenda ya Taifa. Lazima tutafsiri maendeleo ya Tanzania kwa miaka 30 au 50, tuwe na vitu tunaita maendeleo.

“Kama hatujafanya hivi, tuna hatari kwa sababu Katiba yetu inampa nafasi kila rais anayeingia madarakani kwa namna yake, kwa hekima yake na kwa namna ya kutafsiri yeye maendeleo ya Tanzania,” amesema Askofu Gwajima.

Akichangia bungeni hapo, Askofu Gwajima amehoji, nchi inawezaje kusonga mbele wakati hakuna muendelezo wa mikakati na juhudi za waliotangulia?

error: Content is protected !!