December 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nape: Kukosoa ni silaha, si udhaifu

Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama (CCM)

Spread the love

 

NAPE Nnauye, Mbunge wa Mtama (CCM), amesema kwa mujibu wa chama hicho, tabia ya kukosoa na kujikosoa ni silaha ya mapinduzi na kujiimarisha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akichangia makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake kwa mwaka 2021/22, Nape amesema, kufanya hivyo si si dalili ya udhaifu.

“Tusigombane bila sababu, Tanzania ni yetu sote, tumsaidie mama (Rais Samia Suluhu Hassan) naye aandike kitabu chake, tusimshike mkono kumwandikia kitabu,” amesema Nape akisitiza kauli ya Rais Mstaafu, Alhaji Ali Hassani Mwinyi “kila zaman a kitabu chake.”

Nape amesema, alama aliyoiacha Hayati John Magufuli itajitetea yenyewe, na kwamba labda kama kuna mtu ana mashaka na alama yake.

“…lakini kama hakuna mashaka na legacy (alama) yake itasikilizwa, itaongelewa sisi Watoto, wajukuu na vitukuu kwa sababu, haya waliyoyafanya watayakuta,” amesema Nape.

Nape ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM amesema, Rais Samia ameanza vizuri ambapo amewataka Watanzania kumuunga mkono.

error: Content is protected !!