May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Flaviana: Siendi kujifunza TLS

Spread the love

 

WAKILI Flaviana Charles, mgombea pekee mwanamke kati ya watu watano waliojitosa kusaka kiti cha Urais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), amesema ana uzoefu wa kuongoza chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha….(endelea).

Flaviana amesema hayo leo Alhamisi tarehe 15 Aprili 2021, akizungumza na wanahabari jijini Arusha.

TLS kinatarajia kufanya uchaguzi wa urais kesho Ijumaa tarehe 16 Aprili 2021, watakaochuana ni, Dk. Edward Hoseah, Francis Stolla, Shehzada Walli na Albert Msando.

Akizungumzia uchaguzi huo, Flaviana ameomba wanachama wa TLS wamchague kwa kuwa yeye si mgeni ndani ya chama hicho, hivyo atakwenda kufanya kazi badala ya kutumia muda mrefu kujifunza uongozi wa chama hicho.

Mwanamama huyo aliwahi kuwa Makamu wa Rais wa TLS kwa muda wa miaka mwili.

Dk. Rugemeleza Nshala, Rais wa TLS anayemaliza muda wake

“Mimi siji kujifunza, naingia kwenye chama nikiwa mwenyeji, niliwahi kuwa kiongozi TLS nakuja na uzoefu ambao utakisaidia chama.

” Uongozi wenyewe ni wa mwaka mmoja, ukichagua ambaye hajawahi kuwa ndani atakuwa na miezi sita ya kujifunza,” amesema Flaviana.

Kuhusu ushindani kwenye uchaguzi huo, amesema upo lakini anaamini atashinda.

“Namshukuru Mungu sababu ninaona ni watu wengi wa kuniunga mkono. Watu wengi wamesimama na mimi na naona mchakato unaenda vizuri.

” Unaposimama kama mwanawamke kuna changamoto mnaona kulivyo na ushindani mzuri naweza kujitathimini kwamba naongoza naamini nitashinda,” amesema Flaviana.

error: Content is protected !!